MAKONDA AKABIDHIWA PIKIPIKI ZA MILIONI 400

Date:

Share post:

KAMPUNI ya TONGBA ya China inayojihusisha na utengenezaji pikipiki, leo imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pikipiki 10 za kisasa.

Pikipiki hizo zenye thamani y ash. Milioni 400 ni maalumu kwa ajili ya kutumiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo jijini Dar es Salaam, Makonda alisema aliiomba TONGBA msaada wa pikipiki za kisasa kwa ajili ya askari wa usalama barabarani ili kukiongezea uwezo kikosi hicho katika utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema kupatikana kwa pikipiki hizo kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani wanapoongoza misafara ya viongozi, misiba na kuwahisha wagonjwa waliozidiwa hospitalini.

“Lengo langu ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi, natamani kuona askari wana vifaa vya kutosha. Hadi sasa tumepata baiskeli 500, pikipiki za kawaida 200, kompyuta 100, pikipiki kwa ajili ya askari wa usalama barabarani na matengenezo ya magari,” alisema Makonda.

Wakati huo huo, Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata askari wote waliobainika kushirikiana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya na wanaobambikia wananchi kesi ndani ya muda wa saa tano.

Agizo hilo la Makonda limekuja baada ya juzi kupatiwa taarifa za mmoja wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aliyekuwa mikononi mwa polisi kutoweka katika mazingira yasiyoeleweka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, muuza unga huyo baada ya kutoweka mikononi mwa polisi alirudi katika hoteli aliyokamatwa na kufanya fujo huku akihoji aliyetoa taarifa zake na Makonda baada ya kupatiwa taarifa na kufika eneo la tukio na kuagiza awashiwe kamera za CCTV kuangalia kulichotokea ambapo polisi waliohusika walionekana.

“Pia wapo askari waliomkamata mwananchi akiwa na mpenzi wake kwenye gari, wakawapiga picha za utupu na kuwalazimisha watoe Sh. milioni tano ili wasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume sheria.

“Hatuwezi kuruhusu vitendo hivyo hapa mkoani. Ni lazima sheria na haki vitendeke kwa wananchi,” alisema Makonda.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa alisema wapo askari Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanaoshirikiana na raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori ambao uchunguzi utakapokamilika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...