BEIJING, China
INJINI kukatishiwa mzunguko wa mafuta ndiyo chanzo cha ajali ya ndege aina ya Boeing 737 iliyotokea mwaka 2022 nchini China.
Majibu hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa na Bodi ya Usalama wa Sekta ya Usafiri ya Marekani (NTSB).
Ni kwa maana, NTSB inathibitisha madai ya awali, kwamba ajali hiyo ilisababishwa kwa makusudi.
Katika ripoti yake, NTSB imeeleza kuwa kasi ya injini ya ndege hiyo ilipungua ghafla baada ya kusitishiwa mfumo wa kufikiwa na mafuta.
Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya abiria 132, inatajwa kuwa ndiyo kubwa zaidi ya usafiri wa anga ya China kwa miaka 10 ya hivi karibuni.
Hata hivyo, wakati NTSB ikiibuka na madai hayo, bado China haijatoa ripoti yake ya mwisho juu ya chanzo cha ajali.






