BEIJING, China
MLIPUKO uliotokea katika kiwanda cha utengenezaji wa fataki umesababisha vifo vya watu 21 na kujeruhi wengine 61.
Kwa mujibu wa taarifa, tukio hilo limetokea jana Mei 4, 2026 katika Jimbo la Hunan mjini Liuyang.
Mamlaka za Liuyang zilitumia wataalamu wa uokoaji takribani 500 kuendesha zoezi la kutafuta walionasa kwenye jengo la kiwanda hicho.
Kwa upande mwingine, majeruhi wa mlipuko huo wametajwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 20 hadi 60.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mlipuko huo.






