TANAPA YAZIDI KUJIIMARISHA KIUTENDAJI, YAAPISHA MAKAMISHNA WAPYA WA UHIFADHI JIJINI DODOMA

Date:

Share post:

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaendelea kuimarisha mfumo wake wa uongozi na utendaji kazi kwa kuwapandisha na kuwaapisha viongozi wapya wa ngazi mbalimbali za uhifadhi, katika hatua inayolenga kuongeza ufanisi na tija katika uhifadhi wa rasilimali za taifa.

Hatua hiyo imefanyika tarehe 25 Aprili 2026 katika Ofisi Kiunganishi za TANAPA zilizopo jijini Dodoma, ambapo jumla ya maafisa watano wameapishwa na kuvishwa vyeo vipya.

Walioapishwa ni pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi mmoja (1), Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi watatu (3), pamoja na Afisa Uhifadhi Mkuu mmoja (1).

Uongozi watakiwa kufanya kazi kwa weledi na kujituma
Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Musa Nassoro Kuji, aliwataka makamishna hao wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uadilifu, huku wakizingatia viapo walivyoapa.

Alisisitiza umuhimu wa viongozi kusikiliza maoni ya watendaji walio chini yao kama njia ya kuongeza ufanisi wa kazi na kufanikisha malengo ya Shirika pamoja na maslahi mapana ya Taifa.

“Nendeni mkachape kazi kwa bidii na weledi huku mkiishi viapo mlivyoapa leo. Kiongozi mzuri ni yule anayesikiliza mawazo ya watu wake, hivyo sikilizeni mnaowaongoza,” alisema Kamishna Kuji.

Shukrani zatoa ujumbe wa matumaini
Kwa upande wake, akizungumza kwa niaba ya wenzake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Bw. Abdallah Omary Kiwango, aliishukuru Bodi ya Wadhamini pamoja na Uongozi wa TANAPA kwa kuonesha imani kwa kuwapa nafasi ya kulitumikia Shirika katika nyadhifa hizo mpya.

Waliopandishwa vyeo katika hafla hiyo ni:

Abdallah Omary Kiwango – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi
Philbert Michael Ngoti – Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
Joachim Shaaban Tesha – Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
Michael Joseph Tarimo – Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
Manendo Peter Maziku – Afisa Uhifadhi Mkuu

TANAPA inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuimarisha utendaji kazi na uongozi bora ili kuhakikisha hifadhi za taifa zinasimamiwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MWENGE WAANGAZA MATUMAINI YA AJIRA KWA VIJANA MKURANGA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda, amezindua mradi wa basi dogo unaoendeshwa na...

DKT MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI WA BARA NA VISIWANI KUJADILI MUUNGANO

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameongoza Kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na...

RAIS SAMIA AZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI BAHARI KUU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Samia amezindua meli hiyo leo Aprili 25,2026 kwenye ufukwe wa Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi nchini...

JELA MIAKA 30 KWA KUPATIKANA NA BANGI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu Brown Frank Mwaitubi (31), mkazi wa Kajunjumele, kifungo cha miaka...