DK. GWAJIMA AKEMEA IMANI POTOFU KUHUSU NYETI

Date:

Share post:

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy  Gwajima, amekemea uzushi unaoenezwa na baadhi ya watu wenye nia ya kupotosha jamii kuwa mwanaume akishikwa bega hupoteza sehemu zake za siri (Nyeti)

Dk. Dorothy amekemea uzushi huo jana, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto Anayeishi na Kufanya Kazi Mtaani yaliyofanyika katika Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar Es Salaam, yaliyolenga kuhamasisha ulinzi, malezi na ustawi wa watoto.

Akizungumzia hali hiyo,  Gwajima aliendesha zoezi la wanaume kushikana mabega, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, ili kuthibitisha ukweli wa madai hayo ambapo mara baada ya zoezi hilo, wanaume walithibitisha kuwa taarifa hizo ni za uongo, kwani hakuna aliyepotelewa nyeti zake.

Aidha, Dk. Dorothy amewataka wananchi kupuuza uzushi huo na badala yake wajikite katika shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii huku akisisitiza umuhimu wa kujenga jamii yenye uelewa sahihi inayoweza kupambanua taarifa za kweli na za upotoshaji ili kuimarisha maendeleo endelevu ya taifa.

Amewaelekeza viongozi wa Wizara hiyo kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa jamii ili kuondoa dhana potofu hiyo, akisisitiza kuwa upotoshaji wa aina hiyo unalenga kupunguza umakini wa wananchi katika ajenda za maendeleo na ustawi wa jamii.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...