DKT KIJAJI: UHIFADHI ENDELEVU NI INJINI YA UKUAJI WA UTALII NCHINI

Date:

Share post:

Viongozi wa jamii kutoka wilaya za Longido na Ngorongoro wamekutana na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma kwa lengo la kuimarisha uelewa wa pamoja kuhusu uhifadhi endelevu wa rasilimali za asili na namna unavyoweza kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema kuwa utunzaji wa maliasili ni mhimili muhimu wa ukuaji wa sekta ya utalii, akisisitiza kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiwango kikubwa mapato ya taifa na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira kwa Watanzania wengi.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa fedha zinazopatikana kupitia utalii zimekuwa zikiwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, huduma za afya, elimu, maji safi na miradi ya kijamii katika maeneo mengi nchini.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha uhifadhi wa mazingira unaendana sambamba na maendeleo ya kiuchumi, huku akitoa wito kwa jamii zinazoishi maeneo ya hifadhi kuwa sehemu ya ulinzi wa rasilimali hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

“Uhifadhi endelevu si kwa ajili ya wanyama pekee, bali ni msingi wa uchumi wetu na maendeleo ya jamii zetu,” alisema Dkt. Kijaji.

Katika kikao hicho, Waziri Kijaji aliahidi kuwa wizara itaendelea kushirikiana na viongozi wa jamii katika kulinda rasilimali za asili na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wananchi ili kuzuia uharibifu wa mazingira na vitendo vinavyohatarisha ustawi wa maliasili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, Mhe. Thomas Ngobei, aliahidi ushirikiano wa dhati katika juhudi za uhifadhi hususan katika mchakato wa kuanzisha Hifadhi ya Jamii ya Ziwa Natron (JUHIZINA), akisisitiza kuwa jamii itaendelea kushiriki katika ulinzi wa mazingira kwa maslahi mapana ya taifa.

Katika hatua nyingine, Waziri Kijaji alikutana na uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kuwataka kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao ili kufikia malengo ya serikali katika kukuza utalii na kuimarisha usimamizi wa hifadhi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wataalamu mbalimbali wa sekta hiyo.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...