HANDENI WAKUTANA KUJIPANGA KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Date:

Share post:

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amefanya kikao maalum cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2026, kikilenga kujadili namna bora ya kuupokea na kuuenzi Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Handeni.

Katika kikao hicho, imeelezwa kuwa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili tarehe 18 Juni 2026 katika Halmashauri ya Mji wa Handeni na tarehe 19 Juni 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Nyamwese amesema kuwa Mwenge wa Uhuru si mgeni kwa wananchi wa Handeni bali ni alama muhimu ya Taifa, inayobeba ujumbe wa mshikamano, maendeleo na matumaini kwa Watanzania wote.

“Mwenge wa Uhuru ni alama na tunu ya Taifa letu. Unamulika, unaelimisha, kuhamasisha maendeleo ndani na kutoa matumaini ndani na nje ya mipaka ya nchi,” amesema DC Nyamwese.

Aidha, amewataka viongozi na watendaji wote kushirikiana kikamilifu kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati ili Wilaya iweze kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa mafanikio makubwa.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge kwa Mwaka 2026 inasema  “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...