TANZANIA INALO KANISA KATOLIKI LENYE MIAKA 145  

Date:

Share post:

UKITAKA kuliona au kusali ndani ya Kanisa Katoliki la kihistoria lenye miaka  zaidi ya 145 tangu lilipojengwa, nenda katalii kwenye makumbusho ya Dkt. David Livingstone, iliyopo Manispaa ya Ujiji – Kigoma, Mkoa wa Kigoma.

Kanisa hilo la kihistoria lililojengwa mwaka 1879 na wakoloni wa kijerumani; hadi sasa linatumiwa na waumini wengi wa dini ya kikristu kutoka ulimwengu kote kuabudu huku watalii wengi kutoka Ulaya na Marekani wakienda hapo kutalii na kupiga picha.

Ni moja ya majengo yaliyosanifiwa na mabingwa wa usanifu majengo wa mwashoni mwa karne 18 na limejengwa kwa ustadi mkubwa, likiwa na nguzo imara ambazo hazina nondo.

Mariam Mkonya, Mhifadhi Mkuu wa Malikale, Makumbusho ya Dkt. David Livingstone, iliyopo Ujiji, Kigoma akiwa amesimama mbele ya Kanisa Katoliki lililojengwa mwaka 1879, akielezea historia ya kanisa hilo.

Mhifadhi Mkuu wa Malikale, Makumbusho ya Dkt. David Livingstone, Miriam Mkonya, anasema katika Bara la Afrika, majengo ya aina hiyo yaliyopo sasa ni machache sana na yamekuwa yakitumiwa na wataalamu wa usanifu majengo, hususan kutoka Ulaya na Marekani kujifunza utaalamu wa usanifu majengo waliokuwa nao wasanifu majengo wa karne ya 18 na 19.

Anasema wataalamu wa usanifu mejengo wa hapa nchini na Afrika Mashariki wanaweza kupata elimu ya ziada ya usanifu majengo kwa kulitembelea kanisa hilo.

Ndilo kanisa la kwanza kujengwa katika Mkoa wa Kigoma na Padre wa kwanza wa kanisa hilo alitoka Australia.

Kanisa Katoliki la kihistoria lililopo Ujiji, Kigoma lililojengwa mwaka 1879 linavyoonekana kwa ndani.

Tanzania ina hazina kubwa ya urithi wa utamaduni ambao kwa hakika Watanzania wanapaswa kuufikia na kujionea pamoja na vivutio vingine, chimbuko la ukatoliki katika Mkoa wa Kigoma.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...