RIPOTA PANORAMA
RAIS wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma amefariki duniani leo akiwa na umri wa miaka 95.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Windhoek, Nujoma amefariki dunia akiwa hospitalini alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki tatu.
Akitangaza kifo hicho, Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba amesema mauti yalimkuta Najumo katika Mji Mkuu wa Namibia, Windhoek.
Nujoma aliongoza vita vya kudai uhuru wa Namibia ambao ulipatikana mwaka 1990 na yeye kuwa rais wa nchi hiyo pia mwenyekiti wa Chama cha South West People Organisation (Swapo.)
Alikuwa Rais wa Namibia kuanzia mwaka 1990 hadi 2005 alipong’atuka na kubaki kuwa Mwenyekiti wa Swapo hadi mwaka 2007 alipong’atuka akiwa amekiongoza chama hicho kwa muda wa miaka 47.