Nigeria
MCHUNGAJI na bibi harusi ni miongoni mwa watu takriban 20 waliotekwa nyara siku ya jumapili nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya nchini humo, watru hao walitekwea nyara katika matukio mawili tofauti yaliyofanywa na maharamia waliokuwa na silaha za moto.
Taarifa zimeeleza kuwa watekaji walivamia makanisa ya Cherubim na Seraphim yaliyopo jimbo la kati la Kogi kisha wakawalazimisha waumini kulala chini baada ya kufyatua risasi hewani.
Kwamba, katika tukio la kwanza, watekaji walimkamata mchungaji, mkewe na baadhi ya waumini na katika tukio la pili walilolifanya Jimbo la Sokoto Kaskazini, wsaliwakamata bibi harusi na wasimamizi wake.
Mamlaka nchini Nigeria zimekuwa katika mapambano makali dhidi ya makundi ya watekaji ambayo yamezua hofu kwa jamiii.
