Monday, December 23, 2024
spot_img

ISRAEL YAMTISHA KIONGOZI MPYA WA HEZBOLLAH

MASHIRIKA YA KIMATAIFA

WAZIRI wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant ametuma ujumbe kwenye mtandao wa X unaoeleza kuwa uteuzi wa kiongozi mpya wa kundi la Hezbollah la Lebanon, Sheikh Naim Qassem ni wa muda, sio wa kudumu.

Gallant ametoa ujumbe huo mtandaoni muda mfupi baada ya Sheikh Qassem kutangazwa leo na kundi la Hezbollah kuwa kiongozi wake mpya.

Sheikh Qassem anachukua nafasi ya aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah ambaye aliuawa kwenye shambulio la anga la Jeshi la Israel lililofanywa katika Jiji la Beirut, mwezi uliopita.

Kiongozi mpya wa kundi la Hezbollah la Lebanon, Sheikh Naim Qassem.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya kimataifa, kauli ya Gallant inaashiria kuwa maisha ya Sheikh Qassem sasa yako shakani kwani Jeshi la Israel limeua idadi kubwa ya viongozi wa kundi hilo, wiki chache zilizopita.

Sheikh Qassem ni mmoja wa viongozi wachache wa kundi la Hezbollah waliosalia hai baada ya Jeshi la Israel kuua viongozi wengi wa kundi hilo katika mfululizo wa mashambulizi linayofanya.

Kwa zaidi ya miaka 30, Sheikh Qassem alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Kundi la Hezbollah na mmoja wa watu waliotambulika zaidi katika kundi hilo.

Sheikh Qassem ametangazwa kuwa kiongozi wa kundi la Hezbollah akiwa hafahamiki alipo huku baadhi ya ripoti zikionyesha kuwa ameficha nchini Iran akihofia kuangamizwa na majeshi ya Israel.

 .

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya