Monday, December 23, 2024
spot_img

MADAKTARI WASAIDIA KUFA MUME NA MKE

WANANDOA Jan aliyekuwa na umri wa miaka 70 na Els   aliyekuwa na umri wa miaka 71 wamefariki dunia mapema mwezi Juni, 2024 baada ya madaktari nchini Uholanzi kuwapa dawa za kuwasaidia kufa kwa hiari yao wenyewe.

Tukio la kufa kwa hiari kwa wanandoa hao wawili walioshi pamoja kwa takriban miongo mitano limeripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali vya kimataifa kuwa, pumzi zao zilikatishwa na dawa aina ya duo – authanasia.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti tukio hilo kuwa siku tatu kabla marehemu wanandoa hao hawajasaidiwa kufa, walifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa shirika hilo katika eneo la Friesland, lililopo Kaskazini mwa Uholanzi.

BBC imeripoti kuwa marehemu wanandoa hao ambao sehemu kubwa ya maisha yao waliishi kwenye makazi yaliyotengenezwa kwenye boti au kwenye gari, walieleza kuwa wakati mwingine walijaribu kuishi kwenye lundo la mawe lakini walishindwa.

Inaripoti kuwa Els aliyekuwa na matatizo ya akili alipata wakati mgumu kuzungumza wakati wa mahojiano hayo lakini Jan ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo alieleza kuwa kwa maumivu aliyonayo na ugonjwa wa mkewe Els, walipaswa kufa.

Jan na Els walioacha mtoto mmoja wa kiume, kwa mara ya kwanza walikutana katika shule ya chekechea na tangu hapo hawakuachana hadi Juni, 2024 walipokufa pamoja.

Sheria za Uholanzi zinaruhusu madaktari kuwasaidia kufa watu wanaomba kufa kwa hiari yao wenyewe na Jan na Els walijiunga na shirika la kutetea haki za kufariki la Uholanzi kabla ya kutimiza azma yao ya kufa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya