TPA YAFUNGUA OFISI MALAWI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo imefungua rasmi ofisi zake katika Jiji la Lilongwe, Malawi.

Kufunguliwa kwa ofisi hizo kunalenga kuboresha utoaji huduma kwa wateja wa Bandari ya Dar es Salaam walioko nchi jirani.

Taarifa ya kufunguliwa kwa ofisi hizo iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa kwa Tanzania PANORAMA Blog, imeeleza kuwa kunadhihirisha dhamira ya Bandari ya Dar es Salaam kutoa huduma bora kwa wananchi wa Malawi.

Mbossa amesema Malawi ambayo imeunganishwa na ardhi ni miongoni mwa nchi saba zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya nchi hiyo.

Ametaja wateja wengine wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa ni nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Rwanda, Burundi, Uganda na Zimbabwe.

“Jukumu kubwa la uuzaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, hususan Bandari ya Dar es Salaam sasa litakuwa kwenye ofisi iliyofunguliwa Malawi,” amesema Mbossa.

Alizitaja baadhi ya huduma ambazo zitatolewa na ofisi hiyo iliyofunguliwa Jijini Lilongwe, kuwa ni pamoja na kuwapa taarifa mpya ya miradi mipya na  inayoendelea kutekelezwa nchini, mifumo na vifaa pamoja na kupokea malalamiko ya wateja,  wamiliki wa mizigo wa nchini Malawi.

Mbossa amesema Malawi ni mteja namba nne kwa ukubwa wa Bandari ya Dar es Salaam ikitanguliwa na nchi za DRC, Zambia, Rwanda na Burundi na shehena ya mizigo ya nchi hiyo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam iliongezeka kwa asilimia 18.3, mwaka 2022, ikiwa ni tani 557,826.         

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...