MRAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA IMF

Date:

Share post:

TERESIA MHAGAMA NA GODFREY MWEMEZI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jens Reinke kuhusu mwenendo wa uchumi, utekelezaji wa bajeti, mipango ya maendeleo na program ya ufadhili  wa miradi (ECF).

Mhandisi Mramba na Reinke wamekutana leo jijini Dodoma na kikao chao kilihudhuriwa pia na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Mussa Makame na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na wa TPDC.

Katika kikao hicho, Mhandisi Mramba aliwaeleza watendaji hao kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika, ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115, unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024.

Mhandisi Mramba amesema majadiliano baina ya Serikali na wawekezaji wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG) kuhusu mkataba wa nchi hodhi (HGA) na mkataba wa uzalishaji na ugawanywaji mapato (PSA), yamekamilika.

Vilevile, ameeleza kuwa mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ni mzuri.

Ameeleza pia hatua zinazochukuliwa sasa na Serikali kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili ifikapo mwaka 2033, asilimia 80 ya wanachi wawe wanatumia nishati hiyo.

Mhandisi Mramba amekieleza kikao hicho kuwa Tanzania ina vyanzo vya kutosha vya nishati jadidifu ikiwemo jua na upepo vinavyoweza kutumika kuzalisha umeme.

Aidha, ameishukuru IMF kwa kutoa Shilingi bilioni 200, kupitia mpango wa ECF kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuimarisha Gridi ya Taifa pamoja na kupeleka umeme katika vitongoji vya mikoa ya Songwe na Kigoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini Tanzania, Jens Reinke amemshukuru Mhandisi Mramba kwa kumpatia taarifa muhimu  ambazo yeye na wadau wengine zitawasaidia kufahamu mwelekeo wa Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

MATUKIO KATIKA PICHA

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiwa katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo pichani) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke (hayupo pichani).

Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja (wa kwanza kushoto) pamoja na watendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiwa katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo pichani) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke (hayupo pichani).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (wa tatu kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke (wa nne kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na IMF baada ya kikao kilichofanyika jijini Dodoma, lem.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NEWCASTLE KUMUUZA MSHAMBULIAJI WA BEI MBAYA

LONDON, UingerezaKLABU ya Newcastle United itampiga bei straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Yoane Wissa,...

LIVERPOOL NAYO YAJITOSA KWA WHARTON

MERSEYSIDE, UingerezaLIVERPOOL imeungana na klabu zingine kubwa za Ulaya zinazomtolea macho kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton. Mtandao wa...

SINTOFAHAMU KUELEKEA MAZUNGUMZO YA PILI KATI YA MAREKANI, IRAN

WASHINGTON DC, MarekaniAKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Aprili 16, 2026, Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema ana matumaini...

TAJIRI WA MAN CITY ANAHUSIKA VIPI VITA NCHINI SUDAN?

MANCHESTER, UingerezaMMILIKI wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed Al-Nahyan, anakabiliwa na tuhuma nzito za kusambaza...