Klabu ya KVC Westerlo imemtambulisha rasmi David Amegnaglo kama mchezaji wake mpya kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Katika ujumbe huo, klabu hiyo iliwakaribisha mashabiki wake kumpokea kwa furaha nyota huyo mpya, ikisema: “Tumpokee kwa ukarimu mchezaji wetu mpya, David Amegnaglo.”

Usajili wa Amegnaglo unatarajiwa kuimarisha kikosi cha KVC Westerlo kuelekea msimu mpya, huku mashabiki wakisubiri kumuona akianza kuitumikia klabu hiyo katika mashindano mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here