KAMISHENI YA TUME YA MADINI YA RIDHISHWA NA KASI YA UKUSANYAJI WA MADUHULI, SEKTA YA MADINI NCHINI

Date:

Share post:

Kamisheni ya Tume ya Madini imeridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa maduhuli katika Sekta ya Madini kupitia Tume ya Madini, hatua inayotoa matarajio ya Serikali kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Hayo yamebainishwa leo Mei 4, 2026 jijini Dodoma wakati Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo, alipoongoza kikao cha Kamisheni kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Lekashingo amewapongeza watendaji wa Tume ya Madini kwa mafanikio yaliyopatikana hususan katika ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini, kuimarika kwa usalama migodini pamoja na kuongezeka kwa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini.

“Nina imani kwa kasi iliyopo tutavuka lengo la Serikali la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka huu wa fedha. Kazi inayofanywa na watendaji wa Tume inaonesha dhamira ya dhati ya kukuza Sekta ya Madini,” amesema Dkt. Lekashingo.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Tume imeendelea kusimamia utoaji na ufuatiliaji wa leseni za madini, ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, usimamizi wa uzalishaji na mauzo ya madini pamoja na utekelezaji wa majukumu ya kisheria katika sekta hiyo.

Pia ameongezaTume imefanya kaguzi katika migodi mikubwa, ya kati na midogo, mitambo ya uchakataji na uchenjuaji wa madini, mabwawa ya kuhifadhi tope sumu, maeneo ya miambataka na maghala ya kuhifadhi baruti katika mikoa yote ya kimadini nchini kwa lengo la kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia usalama, afya na utunzaji wa mazingira.

Aidha, ameeleza kuwa usimamizi wa biashara ya madini umeendelea kuimarika kupitia masoko ya madini 44 na vituo 120 vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini, hatua iliyosaidia kuongeza uwazi wa biashara na kuongeza ufanisi katika mfumo wa uuzaji na usafirishaji wa madini nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RC ARUSHA ATOA RUHUSA MGOGORO WA MWEKEZAJI NA MPANGAJI KARATU KUAMULIWA MAHAKAMANI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, amearuhusu mgogoro kati ya Kampuni ya Tarylin Limited...

WAZIRI MKUU ASISITIZA USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKABILIANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika mapambano dhidi ya uhalifu...

RAIS WA KENYA WILLIUM RUTO AWASILI NCHINI

Rais wa Kenya, William Ruto, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha...

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...