RAIS WA KENYA WILLIUM RUTO AWASILI NCHINI

Date:

Share post:

Rais wa Kenya, William Ruto, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya.

Rais Ruto anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan, leo Mei 4, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao watajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Samia na Rais Ruto wanatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi hizo mbili, kwa lengo la kuimarisha biashara na uwekezaji wa kikanda.

Mapema kesho, Mei 5, 2026, Mheshimiwa Ruto atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kabla ya kuhitimisha ziara yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RC ARUSHA ATOA RUHUSA MGOGORO WA MWEKEZAJI NA MPANGAJI KARATU KUAMULIWA MAHAKAMANI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, amearuhusu mgogoro kati ya Kampuni ya Tarylin Limited...

KAMISHENI YA TUME YA MADINI YA RIDHISHWA NA KASI YA UKUSANYAJI WA MADUHULI, SEKTA YA MADINI NCHINI

Kamisheni ya Tume ya Madini imeridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa maduhuli katika Sekta ya Madini kupitia Tume...

WAZIRI MKUU ASISITIZA USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKABILIANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika mapambano dhidi ya uhalifu...

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...