‘KARIAKOO DERBY’ NA UKAME WA MABAO YA KIPINDI CHA KWANZA

Date:

Share post:

TAKWIMU zinaongea! Hakuna bao lililofungwa katika dakika 45 za kwanza katika mechi zote tano za ‘Kariakoo Derby’ zilizochezwa hivi karibuni.

‘Derby’ iliyopita, ambayo ilikuwa ya fainali ya Kombe la Muungano, ilishuhudia bao pekee la mchezo likifungwa katika dakika ya 120, mfungaji akiwa Seleman Mwalim wa Simba.

Kabla ya hiyo, derby ya Machi Mosi, 2026 haikushuhudia bao, si tu kipindi cha kwanza, bali hata dakika zote 45 za kipindi cha pili. Mechi hiyo ya Ligi ikaisha kwa Yanga na Simba kugawana pointi.

Nyuma yake, ni derby ya Septemba 16, 2025, ambapo bao pekee la mchezo lililoipa Yanga pointi tatu lilifungwa na Pacome Zouzoua katika dakika ya 56.

Mechi hiyo ilitanguliwa na ile ya Juni 25, 2025. Mabao yote ya Yanga katika ushindi wa 2-0 yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa Pacome (dk. 67) na Maxi Nzengeli (dk. 88).

Ya mwisho kati ya hizo tano ni derby ya Oktoba 19, 2025. Yanga ilizoa pointi tatu kwa bao la kujifunga la Kelvin Kijili katika dakika ya 86.

Je, derby ya wikiendi hii itashuhudia nyavu zikitikiswa ndani ya dakika 45 za kwanza au ni mwendelezo wa kusubiri kipindi cha pili?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...