AMA hakika, hilo ndilo swali unaloweza kujiuliza kuelekea ‘Kariakoo Derby’ ya Jumapili ya wiki hii, Mei 3, 2026, itakayochezwa katika Uwanja wa Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.
Katika ‘derby’ mbili za hivi karibuni, ni kama Wekundu wa Msimbazi wamekataa unyonge mbele ya vigogo wenzao hao wa soka la Tanzania.
Mechi mbili ambazo Simba wamegoma kufungwa ni hii ya hivi karibuni (Aprili 29, 2026) iliyochezwa Visiwani Zanzibar. Waliifunga Yanga bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano.
Mchezo mwingine wa derby ni ule wa Machi Mosi, 2026, ambapo kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilipata suluhu (0-0) mbele ya wapinzani wake hao.
Kabla ya mechi hizo za hivi karibuni, Simba ilikuwa imepoteza mara nne mfululizo mbele ya Yanga (1-0, 2-0, 1-0 na 1-0).
Je, katika mchezo wa wikiendi hii Simba itaendelea kujinasua au itarudi kwenye utumwa wake mbele ya wakongwe wenzao?






