SERIKALI YA ZANZIBAR YAONGEZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA HADI LAKI 5

Date:

Share post:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 300,000 hadi kufikia shilingi 500,000 kwa mwezi.

Tangazo hilo limetolewa leo Mei 1, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutekelezwa kuanzia Januari 2027, huku akibainisha kuwa hatua hiyo imelenga kuboresha hali ya uchumi wa wafanyakazi, kupunguza gharama za maisha na kuongeza motisha kazini.

Aidha, Rais Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya kazi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uzalendo ili kuchochea maendeleo endelevu ya Zanzibar.

Hatahivyo, Rais Mwinyi, Amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya Kazi na Uwezeshaji, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (ZATUC) pamoja na Chama cha Waajiri Zanzibar (ZANEMA) katika kushughulikia changamoto za wafanyakazi na waajiri, ambapo changamoto 24 kati ya 29 zilizowasilishwa zimepatiwa ufumbuzi.

Rais Mwinyi pia ametangaza kuwa Serikali imetenga nafasi za ajira 7,500 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza ukosefu wa ajira na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Akihitimisha hotuba yake, ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo, huku akiwahimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi kwa manufaa ya taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...