YALIYOJIRI MKUTANO MKUU WA FIFA

Date:

Share post:

VANCOUVER, Canada
MKUTANO Mkuu wa 76 wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ulifanyika Aprili 30, 2026 mjini Vancouver na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 1,600.

Ni Mkutano uliofanyika kwa mara ya kwanza mjini Vancouver tangu mwaka 2015 na wa mwisho kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazoanza Juni.

Je, ni yapi yaliyojiri katika Mkutano huo? Makala haya yanachambua.

JOTA WA LIVERPOOL AKUMBUKWA
Mbali ya ajenda ya Mkutano, FIFA iliendesha tukio la ukimya wa dakika chache kuwakumbuka watu mbalimbali ndani ya soka waliopoteza maisha.

Miongoni mwao ni staa wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya Ureno, Diogo Jota, aliyepoteza maisha katika ajali ya gari.

IRAN YAHAKIKISHIWA NAFASI KOMBE LA DUNIA
Licha ya Iran kutokuwa na mwakilishi kwenye Mkutano wa jana, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alisema Taifa hilo litashiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Iran imepangwa Kundi D, ambapo mechi zake dhidi ya Ubelgiji, Misri na New Zealand zitachezwa Marekani katika miji ya Los Angeles na Seattle.

Infantino amesema mgogoro unaoendelea kati ya Iran na Marekani inayoshirikiana na Israel hautouzuia nchi hiyo kuwa sehemu ya michuano hiyo.

Alisema: “Iran itashiriki na itacheza mechi zake za Marekani. Tunapaswa kuwaleta watu pamoja. Ni jukumu langu, ni jukumu letu. Soka linaunganisha dunia, FIFA inaunganisha dunia.”

INFANTINHO KUGOMBEA TENA URAIS
Katika Mkutano huo, Infantino mwenye umri wa miaka 56 alitangaza nia yake ya kugombea tena kiti cha urais kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Uchaguzi utafanyika Machi 18, 2027 nchini Morocco. Ni kwa mara ya pili mfululizo FIFA kufanya Uchaguzi wake barani Afrika.

Infantino anataka awamu ya nne madarakani tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kuchukua nafasi ya Sepp Blatter.

Mashirikisho ya soka katika mabara ya Afrika (CAF) na Asia (AFC) yanatajwa kumuunga mkono kwa asilimia 100.

MGOGORO WA PALESTINA, ISRAEL WAIBUKA
Rais wa Shirikisho la Soka la Palestina, Jibril Rajoub, na Makamu wa Rais wa Chama cha Soka cha Israel, Basim Sheikh Suliman, waliibua mjadala mkubwa katika Mkutano huo.

Rajoub aliishutumu Israel kwa kuzipatia fedha klabu za soka zilizoko Palestina na aligoma kupiga picha ya pamoja na Sheikh Suliman hata baada ya kuombwa na Infantino.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...