NI ‘KARIAKOO DERBY’ YA PRINCE DUBE, SELEMAN MWALIM

Date:

Share post:

SIKIA hii! Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara itakayochezwa Jumapili ya wiki hii, Mei 3, 2026, katika Uwanja wa Jenerali Isamuhyo.

Kuelekea mchezo huo wa 20 kwa kila timu msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Yanga wako kileleni mwa msimamo, huku Simba ikiipumulia katika nafasi ya pili.

Baada ya kila timu kucheza mechi 19, Yanga inaongoza Ligi baada ya kukusanya pointi 47, wakati Wekundu wa Msimbazi wamekusanya pointi 42.

Kwa upande mwingine, mechi ya wikiendi hii pale Mbweni inabeba taswira ya vita ya mabao kati ya washambuliaji wawili; Prince Dude (Yanga) na Seleman Mwalim (Simba).

Dube raia wa Zimbabwe ndiye kinara wa mabao kwa upande wa kikosi cha Yanga na Ligi Kuu kwa ujumla, akiwa ameshazifumania nyavu mara nane, pia akiwa ametoa ‘asisti’ mbili.

Kwa upande wa Mwalim, ambaye pia ni mshambuliaji wa Taifa Stars, ndiye mchezaji mwenye mabao mengi (6 na asisti moja) katika kikosi cha Simba kufikia hatua hii ya msimu wa Ligi Kuu Bara.

Hivyo, endapo atafunga mabao mawili katika ‘Kariakoo Derby’ ya Jumapili, si tu atamfikia Dube, bali pia atajiweka kwenye nafasi nzuri ya kukiwania kiatu cha ufungaji bora wa msimu huu wa Ligi.

Mbaya kwake, Mwalim si chaguo la kwanza katika kikosi cha Simba, ingawa kiwango alichokionesha alipotokea benchi katika ‘derby’ ya Kombe la Muungano kinaweza kuwa tiketi ya kuingia ‘first eleven’ Jumapili hii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...