SAME UTALII FESTIVAL YAVUTIA WAGENI HIFADHI YA MKOMAZI

Date:

Share post:

Zaidi ya watalii wa ndani 90 wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali na kufurahia utalii wa ndani, kufuatia uzinduzi wa tamasha la Same Utalii Festival msimu wa tatu lililofanyika katika viwanja vya stendi wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Watalii hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo Mbula, Kisima na Njiro, na kujionea wanyamapori wa aina tofauti, hususan faru weusi, ambao ni miongoni mwa vivutio adimu vinavyovutia wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizindua rasmi tamasha hilo, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Malecela, amesema tamasha hilo ni kichocheo kikubwa cha kukuza utalii wa ndani pamoja na uhifadhi, kwani lina nafasi ya kuibua bidhaa mpya za utalii zitakazosaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za taifa.

Mhe. Malecela amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kufanya utalii wa ndani akisisitiza kuwa gharama zimepunguzwa na miundombinu imeimarika, hivyo kufanya wananchi wengi kuwa na uwezo wa kutembelea vivutio vya utalii kwa urahisi.

“Utalii wa ndani ni muhimu sana kwa sababu unaongeza mapato ya taifa na pia unasaidia wananchi kuifahamu nchi yao na rasilimali zake,” amesema Malecela.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. John Mabula, amesema idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi imeongezeka kwa kiwango kikubwa, kutoka wastani wa watalii 7,800 kwa mwaka hadi kufikia zaidi ya watalii 11,000 kwa mwaka katika kipindi cha 2022 hadi 2026.

Amesema ongezeko hilo linatokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wa utalii katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

Kadhalika, Mabula amesema uwepo wa vivutio na ongezeko la wageni ni fursa kwa wananchi wa Same na maeneo jirani kujiinua kiuchumi kupitia biashara ndogondogo, huduma za usafiri, malazi na ujasiriamali mwingine unaohusiana na utalii.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ameomba uongozi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi kuwapatia mafunzo vijana wa bodaboda kuhusu namna ya kuwahudumia wageni na kutoa mwongozo wa awali kwa watalii, hatua ambayo itasaidia kuongeza kipato chao na kuboresha huduma kwa wageni.

Same Utalii Festival imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha utalii wa ndani, huku Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikitajwa kuwa kivutio kikubwa katika tamasha hilo kutokana na uwepo wa wanyamapori adimu ikiwemo faru weusi na mbwa mwitu, ambao huvutia wageni wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...