MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Simba, Mganda Emmanuel Okwi, amemuibua beki wa kikosi hicho, Fikiri Magoso, baada ya kumtaja katika usajili wa wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao.
Magoso ambaye alikuwa kwenye kilichocheza fainali ya Kombe la Washindi Barani Afrika dhidi ya Stella Abdjan ya Ivory Coast mwaka 1993, alisema Simba wanatakiwa kufanya usajili wa wachezaji watano wa kigeni, akiwamo mshambuliaji mwenye kiwango cha juu kama alivyokuwa nyota wao wa zamani Okwi.
Magoso alisema pamoja na timu yao kufika fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliomalizika hivi karibuni, lakini kikosi chao kilikuwa na mapungufu mengi.
Beki huyo wa zamani wa Simba alisema uongozi wa klabu hiyo unatakiwa kusajili nyota wapya wa kigeni katika idara ya ushambuliaji, kiungo na mabeki ili waweze kufanya vizuri msimu ujao.
Alisema hakuridhishwa na viwango vya wachezaji wa kigeni waliosajiliwa msimu uliopita, hasa idara ya ushambuliaji, kwa kuwa hawakuonyesha ubora wao.
Magoso alisema anahitaji kuona anasajiliwa ushambuliaji mkali ambaye akitengenezewa nafasi mbili anafunga moja.
Alisema msimu uliopita walimkosa mshambuliaji mwenye uchu wa kufunga mabao kama aliyokuwa Okwi, kwani timu ilionekana kitengeneza nafasi nyingi lakini tatizo lilikuwa umaliziaji.
Katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Simba ilishika nafasi ya pili, watani wao wa jadi Yanga wakitwaa ubingwq kwa mara ya nne mfululizo.