TANKI LA MAHARAGE LAUA WANAFUNZI WAWILI MOSHI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA,

Moshi, Kilimanjaro

Wanafunzi wawili wa shule ya Sekondari Kisomachi iliyopo Kata ya Vunjo Mashariki, Tarafa ya Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia baada ya kukosa hewa wakatoa maharage kwenye tenki linalotumika kuyahifadhi.

Wanafunzi hao, Godwin John na Edson Mosha wote wana umri wa miaka 17 na walikuwa wanasoma kidato cha nne, walifariki dunia ijumaa jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa vyombo  ya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa (ACP), Simon Maigwa, wanafunzi hao waliofariki dunia baada ya kuingia kwenye tanki hilo linalotumika kuhifadhia maharage ya shule.

Kamanda Maigwa amesema wanafunzi hao walitolewa kwenye tenki hilo na kukimbizwa Kituo cha Afya cha Kirua, Vunjo ambako ilibainika kuwa walikuwa wameishafariki.

Amesema watumishi watatu wa shule hiyo wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi akiwamo mwalimu mkuu, mwalimu wa zamu na mtunza stoo.

Kamanda Maigwa amesema miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa Mawenzi kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...