DC MURO AWAFUNDA VIJANA MIAKA 58 YA MUUNGANO

Date:

Share post:

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro jana aliongoza maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwafunda vijana kuhusu umuhimu wa umoja katika kongamano la vijana Mkoa wa Singida. DC Muro alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith  Mahenge 

Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano ya Chuo cha Uhasibu Singida ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo umuhimu wa kudumisha Muungano, fursa za uchumi katika Mkoa wa Singida na ushiriki wa vijana katika sensa ya watu na makazi 

Akizungumza katika kongamano hilo DC Muro alisema Tanzania Bara haiwezi kuwa salama kama Tanzania Zanzibar haitakuwa salama kiulinzi, kiuchumi na kijamii 

Alisema wakati dunia ikiungana katika muktadha mbalimbali ni vizuri kwa Tanzania kudumisha Muungano ili kutoa nguvu ya kuleta maendeleo kwa jamii za pande zote mbili


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...