Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ni Mamlaka ya Udhibiti wa Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 3 ya mwaka 2019. Mamlaka hii ina majukumu kadhaa ya kutekeleza kwa mujibu wa sheria iliyoianzisha na hapa ni baadhi ya majukumu hayo, katika kudhibiti usafiri wa ardhini.