MADIWANI MPIMBWE WAHOJI UJENZI WA BARABARA

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoa wa Katavi, limemtaka Meneja wa wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuhakikisha anashughulikia barabara zote zinazotakiwa kutengenezwa.

Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa barabara iliyowasilishwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Mlele, Mhandisi Maneno Makorongo juu ya ukarabati wa barabara za halmashauri hiyo, madiwani wamesema inasikitisha kuona barabara zinashindwa kukamilika kukamilika kwa wakati na nyingine hata hazijaanza ujenzi.

Awali akitoa ufafanuzi, Mhandisi Makorongo amesema tatizo la kuchelewa kukarabatiwa barabara hizo ni changamoto ya uhaba wa wakandarasi, jambo ambalo lilipingwa na Mwenyeketi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Sailas Irumba.

“Kila siku mkandarasi, mkandarasi. Meneja sisi hatutaki hao wakandarasi, nchi hii ina wakandarasi wengi tunataka wananchi wetu Halmashauri ya Mpimbwe waweze kuneemeka na fedha anayoitoa Mheshimiwa Rais kwenye TARURA,”amesema.

Baada ya Mwenyekiti kutoa kauli hiyo, Mhandisi Makorongo aliwaahidi madiwani kuwa atazingatia ushauri uliotolewa na kuufanyia kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...