DRC YAMFUKUZA BALOZI WA RWANDA

Date:

Share post:

CONGO, DRC

JAMHURIi ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemfukuza balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku ikimpa saa 48 kuondoka nchini humo.

Hatua hiyo inakuja wakati kundi la waasi la M23 ambalo Congo inadai linaungwa mkono na Kigali, likiendelea kupata nguvu huko mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Msemaji wa Serikali ya Congo, Patrick Muyaya imesema kutokana na Rwanda kuendelea kuunga mkono M23, baraza la ulinzi linaloongozwa na Rais Felix Tshisekedi limeamua kumpa balozi huyo saa 48 kuondoka nchini humo.

“Hii ni kwa kiasi fulani, kutokana na kuendelea kwa nchi ya (Karenga) kushambulia DRC na kuunga mkono harakati za kigaidi za M23,” imesema taarifa hiyo

Uamuzi wa kumtimua balozi wa Rwanda umefikiwa baada ya Serikali ya Congo kufanya tathmini juu ya hali ya usalama nchini humo.

M23 ni kundi la waasi ambalo mamlaka ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuunga mkono lakini Rwanda inakanusha, liliteka mji wa Kiwanja mashariki mwa Kongo siku ya Jumamosi, na kuukata mji mkuu wa Kivu Kaskazini Goma kutoka nusu ya juu ya jimbo hilo.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...