Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) hawataruhusiwa kuingia katika vituo vya nyuklia vya Iran vilivyoharibiwa na mashambulizi.

“Kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, hakuna mazingira yatakayoruhusu ufikiaji wa maeneo yaliyoshambuliwa na kuharibiwa,” alisema Qalibaf.

Kauli hiyo imekuja wakati Qatar ikitangaza kumalizika kwa duru nyingine ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yaliyofanyika mjini Doha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here