Rais wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kusisitiza msimamo wake kuhusu Mfereji wa Panama, akisema uamuzi wa Marekani kuukabidhi mfereji huo kwa Panama ulikuwa “kosa la kijinga” ambalo halikupaswa kufanywa.
Trump amedai kuwa China inaendelea kuongeza ushawishi wake katika eneo la Mfereji wa Panama na kuonya kuwa hataruhusu hali hiyo kuendelea.
Amesema Marekani ilipaswa kuendelea kuwa na udhibiti wa mfereji huo kutokana na umuhimu wake kwa biashara ya kimataifa na masuala ya usalama.
Kauli hiyo imeibua mjadala mpya kuhusu ushindani wa ushawishi kati ya Marekani na China katika eneo la Amerika ya Kati, huku Trump akiahidi kuchukua hatua za kulinda maslahi ya Marekani na kuzuia kuongezeka kwa ushawishi wa China katika Mfereji wa Panama.






