Wakazi wa Mtaa wa Nyakagwe Kata ya Buhongwa jijini Mwanza, wameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza ( MWAUWASA ), kwa jitihada wanazofanya za kuhakikisha wakazi hao wanapata huduma ya maji kama ilivyokuwa hapo awali.

Mtaa wa Nyakagwe wenye zaidi ya wakazi elfu mbili ulikuwa unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji hali iliyokuwa ikiwalazimu kutumia maji yasiyokuwa salama, lakini baada ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kutua Mwanza na kuagiza huduma hiyo irejeshwe kwa sasa wakazi hao wamerejeshewa tabasamu yao baada ya kupata maji ya uhakika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Maji Mhandisi Mashaka Sitta amewatoa hofu wakazi wa Jiji hilo la Mwanza kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji na kusema watahakikisha maji yanatoka kila eneo huku wakiendelea kuyafanyia kazi marekebisho ya kiufundi yaliyojitokeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here