WAAMUZI WA KIGENI KUCHEZESHA ‘DERBY’, TUNAJENGA AU TUNABOMOA?

Date:

Share post:

UMEANZA kuwa ni utamaduni wa kawaida kwa mechi inayozikutanisha timu kubwa mbili hapa nchini, Simba na Yanga, kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi.

Mwendelezo wake ulishuhudiwa hivi karibuni Visiwani Zanzibar, ambapo mwamuzi wa kati raia wa Kenya, Dickes Nyagrowa, ndiye aliyeamua dakika 120 za fainali iliyozikutanisha timu hizo kwenye michuano ya Kombe la Muungano.

Tujikumbushe; uamuzi wa mamlaka za soka kukimbilia waamuzi wa nje katika mechi za ‘Derby ya Kariakoo’ ulitokana malalamiko ya mashabiki na viongozi wa klabu hizo juu ya waamuzi wa ndani.

Kwamba waamuzi wa ndani si tu hawana uwezo wa kutosha, bali pia wamekuwa wakifanya maamuzi yenye viashiria vya upendeleo.

Wakati fulani, wapo waamuzi waliotajwa kuwa na mapenzi na Simba, kama ambavyo wengine wamekuwa wakihusishwa na upande wa pili, Yanga.

Ilipotokea mwamuzi fulani kupewa derby, basi mashabiki wa upande mmoja wangeibuka na kumkataa, wakidai ni shabiki wa wapinzani wao, hivyo asingemudu mchezo.

Ni katika mazingira hayo, mamlaka za soka haziwezi kukwepa madai kwamba kukimbilia waamuzi wa kigeni kumetokana na kukubaliana na mitazamo ya aina hiyo juu ya waamuzi wa ndani.

Kama si hivyo, basi mamlaka zinakiri kuwapo kwa vitendo vya rushwa na upangaji wa matokeo, ambavyo navyo vimekuwa vikitajwa kuchangia makosa ya makusudi ya waamuzi wa ndani.

Ikimaanisha, mamlaka zimezidiwa na presha iliyopo, hivyo kuona namna pekee ni kuwaridhisha mashabiki na viongozi wa klabu, pasi na kuangalia mustakabali wa waamuzi wa ndani.

Sasa tujiulize; hata kama ni kweli waamuzi wa ndani wana makosa mengi, namna ya kuwajenga ni kuwapokonya mechi zenye hadhi ya juu kama Kariakoo Derby? Na je, mechi wanazopewa kuchezesha ndizo zilizoonekana hazihitaji waamuzi bora?

Bado najiuliza; ikiwa hatua ya kukimbilia waamuzi wa nje inabeba ujumbe kwamba hawa wa ndani hawana uwezo, Chama cha Waamuzi hapa nchini kinatekeleza wajibu wake ipasavyo?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote...

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA WAKUNGA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kuongeza uwekezaji katika mafunzo, ajira, motisha na mazingira ya kazi kwa...

POLISI KUENDELEA KUDHIBITI WAZUSHI MITANDAONI, LIKIIMARISHA ULINZI KUELEKEA DERBY YA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya matukio mbalimbali ya kiusalama na kisheria,...

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UTENGUZI NA UHAMISHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi...