Thursday, 8 October 2026

SHEARER AITABIRIA KIPIGO CHELSEA

LONDON, Uingereza MKONGWE wa Newcastle United, Alan Shearer, anaamini Manchester City itaibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Chelsea. Timu hizo zitaumana kesho Aprili 12, 2026 katika dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) utakaochezwa Stamford Bridge. Chelsea watarejea dimbani wakiwa wametoka kushinda dhidi ya Port Vale, wakati Man City iliifunga […]

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Newcastle United, Alan Shearer, anaamini Manchester City itaibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Timu hizo zitaumana kesho Aprili 12, 2026 katika dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) utakaochezwa Stamford Bridge.

Chelsea watarejea dimbani wakiwa wametoka kushinda dhidi ya Port Vale, wakati Man City iliifunga Liverpool.

Kuelekea mchezo wa kesho, Shearer amesema Man City ya kocha Pep Guardiola ina nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu ikiwa ugenini.

“Man City inahitaji ushindi katika kila mechi, hasa katika mchezo mwingine ujao (wa Ligi) dhidi ya Arsenal,” amesema Shearer.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *