TUME YA JAJI CHANDE YATETA NA DKT. CHAKWERA

Date:

Share post:

MWAKILISHI wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Malawi, Dk.Lazarus Chakwera, amekutana na kufanya mazungumzo na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ujumbe huo wa Jumuiya ya Madola ulikutana na Tume hiyo leo Aprili 11,2026 katika Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es Salaam.

Rais Chakwela amesema ujumbe wake umekuja Tanzania lengo kuu likiwa ni kutafuta suluhisho la kutafuta Suluhu la Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

“Ujumbe wangu umekuja Tanzania kwa lengo la kila mmoja kutafuta Suluhu ya yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi hilo ndilo muhimu kwa sasa mengine nitazungumza baada ya kuhitimisha ziara yangu ya Tanzania,” amesema Chakwera.

Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Othuman Chande, alisema mazungumzo yao yalijikita zaidi kueleza shughuli za Tume hiyo na hadidu za rejea za Tume huku akiwataka waandishi kusubiri taarifa za mjumbe huyo baada ya kukamilisha ziara yake nchini Tanzania.

Mjumbe huyo jana alikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi wa vyama mbalimbali. Bado anaendelea na ziara yake ya kikazi ambayo anataraji kuhitimisha Aprili 16,2026 baada ya kutembelea Zanzibar na Dodoma.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...