Saturday, 22 August 2026

MSIMU WA 4 TUZO MWL. NYERERE ZA UANDISHI BUNIFU KUFANYIKA APRIL 3

HAFLA ya nne ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inatarajiwa kufanyika Aprili 13, 2026, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Super Dome. Akizungumza jijini Dodoma Aprili 8, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema hafla hiyo hufanyika kila mwaka kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Baba wa […]

HAFLA ya nne ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inatarajiwa kufanyika Aprili 13, 2026, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Super Dome.

Akizungumza jijini Dodoma Aprili 8, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema hafla hiyo hufanyika kila mwaka kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, pamoja na kutambua mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Taifa.

Ameeleza kuwa mwaka huu mashindano yamehusisha nyanja nne za fasihi ambazo ni riwaya, hadithi za watoto, tamthiliya na ushairi.

“Tunadhamiria kuendelea kukuza Kiswahili, kuibua na kuendeleza vipaji vya uandishi bunifu, kulinda historia na utamaduni wa Taifa, pamoja na kuongeza hifadhi ya vitabu katika maktaba. Haya ndiyo malengo makuu ya tuzo hii,” amesema Prof. Mkenda.

Ameongeza kuwa geni rasmi wa hafla hiyo ni  mshairi mashuhuri duniani, Abdilatif Abdalla, mwenye asili ya Afrika Mashariki, ambaye aliwahi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 15.

Tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo, jumla ya Watanzania 27 wameshinda.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *