Monday, 24 August 2026

POLISI TISA WAHUKUMIWA KUNYONGWA INDIA

NEW DELHI, India WATUMISHI tisa wa polisi nchini India wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya raia wawili. Mahakama imeeleza kuwa polisi hao waliwaua kwa mateso makali raia wawili waliokuwa waliwashikilia wakati wa janga la Corona mwaka 2020. P Jeyaraj (58), na mtoto wake, 38, walikamatwa na kushikiliwa […]

NEW DELHI, India

WATUMISHI tisa wa polisi nchini India wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya raia wawili.

Mahakama imeeleza kuwa polisi hao waliwaua kwa mateso makali raia wawili waliokuwa waliwashikilia wakati wa janga la Corona mwaka 2020.

P Jeyaraj (58), na mtoto wake, 38, walikamatwa na kushikiliwa na polisi kwa madai ya kufungua duka na kuendelea na biashara wakati wa katazo la kutokutoka ndani (karantini).

Wakiwa mahabusu Kusini mwa Jimbo la Tamil Nadu, taarifa zinaeleza kuwa wawili hao walikumbana na mateso makali kutoka kwa polisi na hatimaye kupoteza maisha.

Itakumbukwa kuwa tukio hilo lilisababisha maandamano makubwa ya raia yaliyoongozwa na wanasiasa wa upinzani.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *