Monday, 24 August 2026

GERRALD ATAKA LIVERPOOL KUMREJESHA LUIS DIAZ KIKOSINI

MERSEYSIDE, Uingereza MKONGWE wa Liverpool, Steven Gerrard, amewataka mabosi wa klabu hiyo kufanya usajili wa haraka ili kuimarisha kikosi chao. Gerrard amependekeza kurejeshwa kwa mshambuliaji wa Liverpool FC aliyeuzwa kwenda Bayern Munich, Luis Diaz. Sambamba na hilo, ameshauri pia kusajiliwa kwa nyota mwingine wa Bayern, Michael Olise, akieleza kuwa anaweza kuziba pengo litakaloachwa na Mohamed […]

MERSEYSIDE, Uingereza

MKONGWE wa Liverpool, Steven Gerrard, amewataka mabosi wa klabu hiyo kufanya usajili wa haraka ili kuimarisha kikosi chao.

Gerrard amependekeza kurejeshwa kwa mshambuliaji wa Liverpool FC aliyeuzwa kwenda Bayern Munich, Luis Diaz.

Sambamba na hilo, ameshauri pia kusajiliwa kwa nyota mwingine wa Bayern, Michael Olise, akieleza kuwa anaweza kuziba pengo litakaloachwa na Mohamed Salah anayetarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Ikumbukwe kuwa Liverpool walimuuza Diaz kwenda Bayern mwaka jana kwa ada ya pauni milioni 65.6.

Licha ya kutumia zaidi ya pauni milioni 400 kuimarisha kikosi, Liverpool bado haijarejea kwenye kiwango chake bora, ikiwa kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa English Premier League.

Wakati huo huo, kiwango cha winga Cody Gakpo kimekuwa cha kupanda na kushuka.

Kwa mujibu wa Gerrard, ujio wa Diaz pamoja na Olise, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 100, unaweza kurejesha makali ya kikosi hicho.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *