Saturday, 10 October 2026

RODRI AZUIWA KUTUA REAL MADRID

MANCHESTER, Uingereza BAADA ya kusikia Real Madrid wanamtaka, mabosi wa Manchester City wamempa ofa ya mkataba mpya kiungo wao raia wa Hispania, Rodri. Mkataba wake na vigogo hao wa jijini Manchester utafikia ukomo mwaka 2027 na taarifa zinaeleza kuwa anataka kuondoka Etihad mwishoni mwa msimu huu. Rodri hajawa kwenye kiwango kizuri tangu alipopona majeraha ya […]

MANCHESTER, Uingereza

BAADA ya kusikia Real Madrid wanamtaka, mabosi wa Manchester City wamempa ofa ya mkataba mpya kiungo wao raia wa Hispania, Rodri.

Mkataba wake na vigogo hao wa jijini Manchester utafikia ukomo mwaka 2027 na taarifa zinaeleza kuwa anataka kuondoka Etihad mwishoni mwa msimu huu.

Rodri hajawa kwenye kiwango kizuri tangu alipopona majeraha ya goti mwaka 2025, ingawa atakumbukwa kwa ubora wake uliompa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024.

Wakati huo huo, Man City wameanza kujipanga na maisha mapya endapo kiungo huyo atakataa kubaki klabuni hapo.

Miongoni mwa viungo inaohusishwa nao kuelekea usajili wa kiangazi ni Elliot Anderson anayefanya vizuri kwa sasa akiwa na kikosi cha Nottingham Forest.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *