Google search engine

JOACHIM LOW KUKABIDHIWA MIKOBA GHANA

Share

IMERIPOTIWA kuwa kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Joachim Low, yuko kwenye mazungumzo na Chama cha Soka cha Ghana.

Kwa mujibu wa ripoti, endapo mazungumzo yatakwenda vizuri, basi kocha huyo atakabidhiwa mikoba ya kuinoa timu ya Taifa hilo ‘Black Stars’.

Taarifa hizo zinaibuka ikiwa imebaki miezi michache kabla ya Ghana kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Kwa upande mwingine, ripoti zinaeleza kuwa kocha huyo atalipwa euro 150,000 kwa mwezi endapo atakubaliana na ofa hiyo.

Ghana haina kocha mkuu tangu Otto Addo alipofungashiwa virago siku chache zilizopota baada ya kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili.

Read more

Local News