Google search engine

ARSENAL MACHO YOTE KWA NYOTA WA REAL MADRID

Share

ARSENAL haijaachana na mpango wake wa kumsajili beki wa Real Madrid, Victor Valdepenas, ingawa inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa AC Milan.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 atawagharimu Washika Bunduki hao kitita cha euro milioni 50.

Licha ya umri wake mdogo, Valdepenas amekuwa akionesha kiwango kizuri kila anapopata nafasi ya kuingia kikosini.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, ni shabiki mkubwa wa Valdepenas akimtaja kuwa ni miongoni mwa vipaji vikubwa kuwahi kutokea katika soka la Hispania.

Ukiziweka kando Arsenal na AC Milan, klabu zingine zilizoripotiwa kumtolea macho ‘dogo’ huyo ni Bayern Munich na Atletico Madrid.

Read more

Local News