Google search engine

LIVERPOOL, UNITED ZATAJIWA DAU LA DIOMANDE

Share

KLABU ya RB Leipzig imetangaza kuwa inahitaji Pauni milioni 87.3 kwa klabu yoyote inayomtaka mshambuliaji wake, Yan Diomande.

Diomande mwenye umri wa miaka 19, amekuwa kwenye rada za vigogo wa Ligi Kuu ya England, Liverpool na Manchester United.

Raia huyo wa Ivory Coast ni moto wa kuotea mbali msimu huu, akiwa amefunga mabao 11 na kutoa ‘asisti’ nane katika mechi 29.

Kwa upande wao, Liverpool wanaamini nyota huyo anafaa kuziba pengo la Mohammed Salah aliyetangaza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, zipo taarifa kuwa saini yake inawindwa pia na klabu zingine kubwa za Ulaya, zikiwamo Bayern Munich, PSG na Tottenham.

Read more

Local News