RAIS WA IRAN KUZIKWA LEO

Date:

Share post:

MASHIRIKA YA KIMATAIFA

RAIS wa Iran, Ebrahim Rais aliyefariki dunia jumapili, Mei 19, 2024 kwa ajali ya helikopta huko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, anatarajiwa kuzikwa leo.

Helikopta iliyokuwa imembeba Rais Raisi ilipata ajali alipokuwa akitokea Mji wa Tasnim, ulio mpakani na Azerbaijan na kuua watu wote aliokuwa akisafiri nao akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir Abdollahian.

Kwa mujibu Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kabla ya kuzikwa, mwili wa Rais Raisi pamoja na aliokuwa akisafiri nao itafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa uchunguzi katika Mji wa Tibriz.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei amekaririwa na vyombo vya habari vya kimataifa akitangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa na amemuidhinisha Makamu wa Rais, Mohammad Mokhber kuwa Kaimu Rais.

Baraza la Mawaziri la Iran limemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ali Baghari Kani kuwa Waziri wa Mambo ya Nje akichukua nafasi ya marehemu Abdollahian.

Rais Raisi alikuwa akitazamwa na wengi kama mtu ambaye angefaa kuchukua nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Iran kutoka kwa Ayatollah Khamenei mwenye umri wa miaka 85 sasa.

Kifo cha Rais Raisi hakitarajiwi kubadilisha mwelekeo wa sera ya Iran au kuitikisa kwa namna yoyote lakini wafuatiliaji wa mambo wameeleza Iran inaweza kuingia majaribuni kutokana na kile kilichoonyeshwa na wapinzani wa Raisi kama ni kushangilia kifo chake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...