UJERUMANI YAWAANGUKIA WATANZANIA

Date:

Share post:

*Yawaomba radhi kwa ukatili iliofanya Vita ya Majimaji

RIPOTA PANORAMA

UJERUMANI imewaangukia watanzania ikiwaomba radhi kwa ukatili iliofanya wakati wa Vita ya Majimaji iliyopiganwa kuanzia mwaka 1905 hadi mwaka 1907.

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Dk. Frank-Walter Steinmeier ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu, amewaomba radhi watanzania leo kwa ukatili waliofanyiwa na wajerumani akiwa mkoani Songea alikotembelea makumbusho ya Vita ya Majimaji.

Rais Steinmeier amesema ipo haja ya kutafuta majibu ya maswali magumu kuhusu vita hiyo ili kujenga uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Ujerumani.

Amesema amejifunza historia ya Vita ya Majimaji na akiwa kwenye makumbusho hiyo aliweka shada la maua kwenye kaburi la halaiki la mashujaa 66 walionyongwa na wajerumani wakati wa Vita ya Majimaji na pia aliweka shada la maua kwenye kaburi la kiongozi wa vita hiyo, Nduna Songea Mbano.

Nduna Songea Mbano

“Vile vile, ana kwa ana, ninaomba msamaha kwa mambo yote ambayo wajerumani waliwatendea mabibi na mababu zenu hapa,” amesema Rais Steinmeier.

Ameeleza furaha yake kujifunza historia ya shujaa Nduna Songea Mbano kwa undani na kukutana na familia yake; na kwamba ameguswa na namna watanzania wanavyohuzunishwa na historia ya mashujaa wao na jinsi ilivyoathiri kizazi cha sasa.

Rais Steinmeier amesema wajerumani wanaoifahamu historia ya Vita ya Majimaji ni wachache hivyo anaibeba kwenda nayo kwao, Ujerumani akawaeleze watu wake historia ya matukio yaliyotokea nyuma ili kuendelea kujenga na kuboresha historia njema ya Tanzania na Ujerumani huko tuendako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...