Tuesday, 6 October 2026

UWEZO WA UZALISHAJI UMEME WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 21

TERESIA MHAGAMA UWEZO wa uzalishaji umeme nchini uimeongezeka kwa asilimia 21.32 huku mahitaji ya sasa, mwaka 2026 yakiwa na ongezeko la asilimia 12.97. Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nishati, Dk. Juma Homera alipokuwa akizindua mifumo ya huduma za umeme kwa haraka na nafuu jijini Dar es Salaam. Amesema huivi sasa taifa lina uwezo wa […]

TERESIA MHAGAMA


UWEZO wa uzalishaji umeme nchini uimeongezeka kwa asilimia 21.32 huku mahitaji ya sasa, mwaka 2026 yakiwa na ongezeko la asilimia 12.97.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nishati, Dk. Juma Homera alipokuwa akizindua mifumo ya huduma za umeme kwa haraka na nafuu jijini Dar es Salaam.

Amesema huivi sasa taifa lina uwezo wa kuzalisha Megawati 4,606 ambazo ni ongezeko la asilimia 21.32 huku mahitaji ya juu ya umeme yakiwa ni Megawati 2,316.

Waziri Homera amesema ongezeko hilo linaenda sambamba na ongezeko la wateja hivyo mifumo mipya ya utoaji huduma aliyoizindua itachangia utekelezaji wa malengo ya serikali, ikiwemo Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayotambua nishati kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.


Dk. Homera amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa inafikapo mwaka 2023 taifa liwe na uwezo wa kuzalisha megawati 8,000 za umeme.

Waziri wa Nishati, Dk. Juma Homera.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dk. James Mataragio, amesema huduma zilizozinduliwa ambazo ni Twiga AI Chatbot, Twiga Premium Customer Portal, Premium Customers Toll Free Line, Premium Customer Service Section pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Wateja ulioboreshwa, ziendane na dhamira ya serikali kuimarisha upatikanaji wa umeme.


About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *