Tuesday, 6 October 2026

‘UJENZI WA RELI YA SGR MAKUTOPORA HADI TABORA UTAKAMILIKA KWA WAKATI’

NASMA MAYUNGA HAKUNA shughuli iliyosimama kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya mwendo kasi, Standard Gauge Rairway (SGR) wala hakuna mabadiliko ya muda wa kukamilika kwa mradi huo. Kil Mtanzania anapaswa kuamini kauli hiyo kwa sababu imetolewa na Mhandisi na Meneja Mradi anayesimamia ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha tatu kinachoanzia Makutopora mpaka Tabora, […]

NASMA MAYUNGA

HAKUNA shughuli iliyosimama kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya mwendo kasi, Standard Gauge Rairway (SGR) wala hakuna mabadiliko ya muda wa kukamilika kwa mradi huo.

Kil Mtanzania anapaswa kuamini kauli hiyo kwa sababu imetolewa na Mhandisi na Meneja Mradi anayesimamia ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha tatu kinachoanzia Makutopora mpaka Tabora, Christopher Kalisti na baadaye ikakaziwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja alipokuwa akitoa taarifa ya mwenendo wa ujenzi wa reli hiyo, kipande cha tatu kinachoanzia Makutopora hadi Tabora.

“Njia kuu ina urefu wa kilomita 294 na njia za mchepuko kilomita 74. Mradi unaendelea vizuri na sasa umefikia asilimia 15.54. Hivi sasa mafundi wapo eneo la Nyahua wanaendelea na ujenzi wa tuta la kutandika reli.

“Vituo vya abiria na mizigo vitakavyojengwa ni Manyoni na Itigi. Vituo vingine vitakuwa kwenye miji midogo midogo ambavyo ni Bula, Goweko, Igalula na kituo kikubwa kabisa kitakuwa Tabora ambacho kitakuwa cha mwisho kwenye kipande hicho cha mradi huo,” anasema Mhandisi Kalisti alipokuwa akitoa akizungumzia maendeleo ya mradi huo hivi karibuni.

Anaeleza zaidi kuwa mradi ukikamilika utarahisisha usafiri kutoka Tabora kwenda mikoa mingine ambayo reli hii itapita. Lakini pia kwa sababu ya reli hii ambayo ni ya kisasa na yenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa, gharama za usafirishaji mizigo zitakuwa nafuu sana.

“Watanzania wanapaswa waelewe kuwa mradi huu wa ujenzi una faida nyingi sana, ikiwemo upatikanaji wa ajira za moja kwa moja na za muda. Wafanyabiashara kutoa huduma mbalimbali mfano kuuza nondo, safuji na maji ya kunywa kwa wafanyakazi.

“Hapo sasa mtu anapaswa kujua kuwa kwa mfano tunaposema wafanyabiashara wanauzia mradi huo nondo; hivyo viwanda zinavyozalisha nondo navyo vimeajiri watanzania wengi tu ambao mradi unaponunua bidhaa unawezesha wao kupata kipato,” anasema Kalisti.

Mradi utakapokamilika utatoa ajitra kwa watanzania na utatoa fursa kubwa ya shughuli za kiuchumi katika vituo vyote ambako kutajengwa maduka kwa hiyo kila Mtanzania anapaswa kujivunia mradi huu.   

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *