Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia, kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Michael Olise, anatarajiwa kukutana na viongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kujadili mustakabali wake.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Real Madrid imeonyesha nia kubwa ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa na ipo tayari kuwasilisha ofa ya takribani euro milioni 225.

Endapo dili hilo litakamilika, litakuwa usajili wa gharama kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya soka.

Hata hivyo, Bayern Munich haijakata tamaa ya kumbakiza Olise, huku ikipanga kumpatia mkataba mpya wenye maslahi makubwa zaidi ya kifedha, ikimtazama kama mmoja wa wachezaji muhimu katika mradi wa muda mrefu wa klabu hiyo.

Iwapo Real Madrid itawasilisha rasmi ofa hiyo, dunia ya soka inaweza kushuhudia rekodi mpya ya usajili, huku hatima ya Michael Olise ikitarajiwa kujulikana baada ya mazungumzo yake na Bayern Munich.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here