Kocha raia wa Ufaransa, Romain Folz, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Ittihad Alexandria, na kuwa kocha wa kwanza kutangazwa rasmi na klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Folz ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika, akiwa amewahi kufanya kazi katika benchi la ufundi la Yanga sports club.
Pia folz amewahi kuhudumu katika timu mbalimbali zenye hadhi barani Afrika ikiwemo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Horoya AC ya Guinea na Pyramids FC ya Misri.
Uteuzi wake unatarajiwa kuipa Al Ittihad Alexandria nguvu mpya katika harakati za kuboresha matokeo na kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya msimu ujao.







