‎Rais wa Marekani, Donald Trump, anatarajiwa kufanya ziara nchini India mapema mwaka ujao, huku Marekani na India zikiendelea kuimarisha uhusiano wao wa kimkakati.

‎Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa Washington na New Delhi ziko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya makubaliano ya kibiashara yanayolenga kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo.

‎Rubio pia amesema kuwa nchi hizo zinaendelea kujiandaa kwa mkutano mwingine wa Quad, jukwaa linalowakutanisha Marekani, India, Japan na Australia kujadili masuala ya usalama na ushirikiano wa kikanda.

‎Trump amekuwa akieleza nia yake ya kuimarisha uhusiano na India, huku akimsifu Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika biashara, diplomasia na usalama wa kimataifa

Imeandaliwa na Mariam Milondomo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here