Friday, 21 August 2026

NEWCASTLE YAKATAA OFA YA ARSENAL YA PAUNI MILIONI 55 KWA BRUNO GUIMAES

Arsenal imepata pigo katika harakati zake za kuimarisha kikosi baada ya Newcastle United kukataa ofa rasmi ya pauni milioni 55 kwa ajili ya kumsajili kiungo Bruno Guimarães. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Arsenal iliwasilisha ofa hiyo siku ya Alhamisi, lakini Newcastle imeweka msimamo kuwa haipo tayari kumuuza nyota huyo wa Brazil kwani ni sehemu muhimu […]

Arsenal imepata pigo katika harakati zake za kuimarisha kikosi baada ya Newcastle United kukataa ofa rasmi ya pauni milioni 55 kwa ajili ya kumsajili kiungo Bruno Guimarães.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Arsenal iliwasilisha ofa hiyo siku ya Alhamisi, lakini Newcastle imeweka msimamo kuwa haipo tayari kumuuza nyota huyo wa Brazil kwani ni sehemu muhimu ya mipango ya klabu kwa msimu ujao.

Imeelezwa kuwa hata kama Arsenal itaongeza ofa hadi pauni milioni 60, bado Newcastle haitafungua milango ya kumuuza Guimarães.

Wakati huo huo, mchezaji huyo anaheshimu uamuzi wa klabu yake, huku Arsenal ikiendelea kutafuta chaguo nyingine za kuimarisha eneo la kiungo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *